Burudani

Lord Eyez apigwa ‘stop’ na Weusi, ni baada ya kudaiwa kuhusika na tukio la wizi

Msemaji kampuni ya Weusi, Nick wa Pili amesema kuwa rapper Lord Eyez amesimamishwa na kampuni hiyo kutokana na kuvunja maadili.
WEUSI_full

Nick wa Pili amesema baada ya kupokea taarifa za Lord Eyez kushikiliwa na polisi huko Arusha kwa wizi wa Laptop walikaa kikao na kuamua kumsimamisha.

“Kitu ambacho naweza kusema kutoka Weusi ni kwamba Lord Eyez tumemsimamisha kazi kikampuni,” Nick ameiambia Bongo5. “Uamuzi wa kumsimamisha tumeufikia jana na leo ndio tumeamua kutangaza rasmi kwamba Lord Eyez tumemsimamisha kazi na amesimamishwa kutokana na misingi na makubaliano ya kampuni,kulingana na maadili ya kampuni yetu na mawazo yetu kwa pamoja ndio yamefanya tukamsimamisha. Kwahiyo ni kwamba tumemsimamisha kutokana na makubaliano ambayo yalifikiwa ndani ya kampuni ambayo mengine yatabakia ndani ya kampuni.”

Uamuzi huo wa Weusi umekuja kufuatia taarifa kuwa Lord Eyez alikamatwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa laptop Jumamosi, huko Arusha na baadhi ya picha za tukio hilo kuonekana. Taarifa hizo zimedai kuwa anatuhumiwa kwa wizi wa laptop aina ya ‘Dell’.

Mwaka juzi, Lord Eyez alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa Power Window za gari la Ommy Dimpoz, lakini Ommy alitangaza kumsamehe msanii huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents