Burudani

Lulu akerwa na headline ya gazeti ‘Mastaa waliozaa watoto wenye sura mbaya’

Muigizaji wa filamu, Elizabeth ‘Lulu’ Michael amekerwa na makala iliyoandikwa na gazeti moja la nchini yenye kichwa cha habari ‘Watoto wa mastaa wenye sura mbaya.’

kalama

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lulu ameandika:

Hivi dunia Imekuwaje!? Hiki kichwa cha habari. Gazeti linalosomwa na mamilioni ya watu unaandika upuuzi kama huu!? Ni basi tu hao watu mliwaandika wana mambo yao mengi….how can u write such a thing!??na gazeti linapita kwa mhariri anaruhusu,linaenda kiwandani mnaangalia tu mpk linatufikia Wananchi…hivi nyie sio wazazi!???au wenzetu mmezaa malaika!???

Kwanza nisifike kwa watoto wenu mana ni malaika wa Mungu tu,wakati mnaandika hii habari mlianza kujiangalia Sura zenu!? Jamani hata kwenye vitabu vya dini watoto wanachukuliwa kama malaika…mmewakosea sana wazazi wao na mmemkosea Mungu zaidi. Mbona kipindi cha Uchaguzi hiki habari ni nyingi.

Mwisho wa siku kama kwako mbaya kwa mzazi wake ni mzuri tu…awe mzuri kwako unachangia hata hela ya kula…!?
MNAJIJUA..

Okay kuna watu mnajaribu kutetea kwamba wametoa kwenye blog kubwa duniani!Okay sawa…Kwani lazima ku copy kila kitu!?? Si tumepewa uwezo wa kuchambua vibaya na vizuri!??? kwahyo ukikuta blog kubwa duniani imekuandikia ukalale na ng’ombe utafanya kwasababu ni blog kubwa duniani!?

Tunaiga Vitu Vizuri jmn..
Excuse ya Blog….No…No…not raiti ?Kwani wamesomea uandishi wa ku copy na ku paste kutoka blog za duniani?vyuo vya uandishi vifungwe basi wakeshe kwenye internet
Nawapa Promo ya 30 minutes na itakuwa deleted Na mm nisiwe nimechangia kupotosha UMMA.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents