Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Habari

Madonna afungua kituo cha upasuaji Malawi

By  | 

Mwanamuziki kutoka  nchini Marekani, Madonna amefungua taasisi itakayoweza kusaidia kufanya upasuaji wa watoto nchini Malawi.

Kituo hicho kimepewa jina la la mtoto wake wa Kike Mercy James Institute, lengo la kuanzishwa taasisi hiyo ni kuhakiksha watoto wa nchi hiyo wanapatiwa matibabu mazuri ili waweze kuwa na afya njema katika ukuaji wao.

Madonna ambaye amekuwa akiwaasili watoto amefanya uzinduzi wa kituo hicho Jumatatu ya wiki hii, kwa mujibu wa kituo cha CNN taasisi hiyo ni kituo cha kwanza kuanzishwa na mwanamama huyo ambaye alifika hapo mwaka 2006 kuanzisha kampeni yake ya “Raising Malawi” ili kusaidia watoto wenye matatizo.

Mwanamuziki huyo ameshawaasili watoto kama Mercy James kisha David Banda na baadae kuwaasili watoto mapacha Esther na Stella.

Na Laila Sued

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW