Habari

Maelfu wapata matibabu bure ndani ya Meli ya Kichina (Picha)

Maelfu ya wananchi wa Dar es Salaam Jumatatu wamejitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya upimaji na matibabu bure ndani ya Meli ya Jeshi la Jamuhuri ya China ambapo katika hali isiyotarajiwa wananchi kutoka mikoani na nje ya Jumuiya ya Africa Mashariki wamesafiri kuja kufuata huduma hiyo.

RC Makonda akizungumza na wananchi waliojitokeza kwa matibabu bure

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewatembelea wananchi hao na kusema kila atakaefika na kupatiwa kadi atapatiwa vipimo, matibabu na dawa Bure na kuwaasa wananchi kutimia vyema fursa hiyo.

RC  amesema madaktari wengine wa China wanaendelea na huduma za matibabu kwenye Hospital za Muhimbili, MOI, Ocean Road, Mwananyamala, Amana na Temeke ili kuhakikisha wanahudumia idadi kubwa ya Wananchi.

Amesema hadi kufikia majira ya mchana tayari Wagonjwa 516 walikuwa wamepimwa na kupatiwa Matibabu jambo linaloonyesha kuwa wananchi wote watapatiwa huduma.

Makonda amesema wapo madaktari bingwa maalumu waliobobea kwa kutoa dawa za kichina kwa wale wagonjwa ambao dawa nyingine zimekuwa zikishindwa kutibu.

Amesema lengo ni kuhakikisha Hakuna mtu anaepoteza maisha kwa kigezo cha kukosa huduma au kumudu gharama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents