Habari

Mahakama yamuhukumu jela mwaka mmoja kwa kumkata mwanaye sehemu za siri

Mahakama ya Wilaya Kalambo mkoa wa Rukwa imemhukumu Esther Mwanisawa (mfipa) miaka 32, mkazi wa kijiji cha katuka wilaya ya Kalambo mkoa wa Rukwa, kifungo cha nje mwaka mmoja na kazi ngumu kwa kosa la kumjeruhi mwanae mdogo wa siku tatu kwa kumkata uume wake.

Mtuhumiwa alishitakiwa kwa kosa hilo kinyume na kifungu 222(b) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya mwaka 2019. Na kutenda kosa hilo Desemba 26, 2019 majira ya 02:00 asubuhi huko katika kijiji cha Katuka wilaya wilayahi humo, ambapo alitenda kosa hilo mara baada ya kujifungua akishirikiana na wanaume wawili ambao walitoweka mara baada ya tukio kutokea.

Hata hivyo mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na upande wa mashitaka ukawa na jukumu la kuthibitisha bila shaka tuhuma zinazomkabili mshitakiwa, huku upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka ASP Mlisho Kimbeho na Ndud Rajabu uliandaa mashahahidi wanne akiwemo mtoto wa mtuhumiwa pamoja na daktari ambao kwa pamoja walithibitha tukio hilo na hivyo mahakama imeona mshitakiwa kuwa na kesi ya kujibu.

Wakati wa ungamo mshitakiwa ameomba mahakama isimpe adhabu kali kwani yeye ni mara yake ya kwanza kufikishwa mahamani na pia ana mtoto mdogo ambaye hajafikisha hta mwaka, na pia ana watoto wengine wanne wanamtegemea.

Akisoma hukumu hiyo hakimu mfawidhi mwandamizi wa mahakama hiyo Mhe.Ramadhani Rugemalira amesema kwa kuzingatia kifungu cha 38 cha sheria na makosa ya jinai sura ya 16 mapitio ya mwaka 2019 na kwa kuzingatia haki ya za watoto hivyo, mahakama imemuhukumu kutumikia kifungo cha miez 12 na kazi ngumu huku ikimuonya kutotenda kosa lolote la jinai katika kipindi cha mwaka mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents