Habari

Mahakama yatupa mbali kesi ya Mbwa Buhari

By  | 

Mahakama nchini Nigeria imeitupilia mbali kesi iliyokuwa inayomkabili mwanaume mmoja aliyempa mbwa wake jina la Rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari.

Mwanaume huyo aliyekuwa akikabiriwa na kesi hiyo, ndugu Joachim Iroko alikamatwa mwaka 2016 baada ya kuripotiwa na jirani yake kwa kitendo hicho ambacho kinaweza kusababisha ghasia kutokana na kutumia jina hilo vibaya.

Baadhi ya watu waliwashutumu Maafisa wa polisi nchini humo kwa kukiuka uhuru uliopo. Hata hivyo mbwa huyo aliuawa kwa madai ya kupewa sumu na watu waliochukizwa na kitendo cha Iroko.

Na Laila Sued

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments