Habari

Makamu wa Rais aanza ziara Pemba

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan jana ameanza ziara ya siku tatu Pemba ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli za maendeleo.

Makamu wa Rais ambaye amewasili Pemba alasiri ya jana na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama ambapo alipokea taarifa za mikoa miwili ya Pemba.

Aidha Makamu wa Rais aliwataka Wananchi wa Chumbageni kukumbuka historia na kurudi nyumbani,aliyasema hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Chumbageni Wambaa.

Leo Makamu wa Rais anatazamiwa kuendelea na ziara yake ambapo ataweka jiwe la msingi katika kituo cha huduma za Mama na Mtoto, Shumba Vyamboni .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents