Habari

Makamu wa Rais akumbuka jambo ambalo Rais Magufuli alilifanya mwaka 2015

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amewataka wa Tanzania kukumbuka kufanya usafi kila Jumamosi ya mwishi wa mwezi huku akimtolea mfano Rais Magufuli kuwa aliahirisha sherehe za uhuru tarehe 9 Disemba mwaka 2015 ili kufanya usafi kwasababu hakuna Uhuru bila afya bora.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo, mjini Dodoma katika uzinduzi wa Kampeni Taifa ya Usafi wa Mazingira awamu ya pili inayobeba jina la ‘Usichukulie poa – nyumba ni choo’ akiwa mmoja wa watu waliohudhuria.

“Rais wetu Magufuli mara kadhaa amesisitiza umuhimu wa usafi, kama ambavyo mnakumbuka aliahirisha sherehe za uhuru 9 Disemba mwaka 2015 ili kila mmoja wetu akiwemo yeye binafsi kushiriki kufanya usafi. Ndugu zangu hili ni jambo kubwa hakuna uhuru bila afya bora,” amesema Samia.

“Kwahiyo alihairisha sherehe zile watu tukafanye usafi, alionyesha mfano mzuri ambao unapaswa kuendelezwa kila kona ya nchi yetu, tumeelekea na zoezi ile lakini imeonekana kama kasi yake imepungua, naomba sana sana sana tuenndeleee na nasisitiza kila Jumamosi ya miwsho wa mwezi kona zote za Tanzania zifanye usafi napenda kuwapongeza sana kama Dodoma na sehemu zote wanazofanya usafi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents