Burudani

Makomando wadai promo ya muziki ni changamoto kubwa zaidi

Kundi la Makomando limesema changamoto kubwa iliyopo kwenye muziki ni promotion ya kazi wanazotoa.

Makomando

Akizungumza na Bongo5 leo, member wa kundi hilo, Fred amesema kundi lao bado linafanya vizuri lakini channgamoto ni budget itakayosaidia kuupeleka muziki wao mbele.

“Kwenye promotion sasa hivi ukitaka kujua unataka kufanya promotion inabidi ujipange sana kwenye suala la budget ili ujue unasambaza vipi kazi yako. Lakini hapo hapo inabidi uamini kazi yako ni nzuri na uamini itapigwa na watu wataipokea. Hata ikipigwa mara moja kama ni nzuri watu wataitafuta. Ndio maana sisi tunajipanga kufanya kazi nzuri ili kupunguza mzigo kwenye masuala ya promo,” amesema Fred.

Katika hatua nyingine Fred amesema wa sasa wanajipanga kuachia kazi mpya itakayowaelimisha vijana kuhusu uchaguzi.

“Sasa hivi tunaandaa kitu cha kuhamasisha vijana waungane kwa pamoja ili tuweze kupiga kura. Sasa tukishamaliza na uchaguzi ukapita nina imani sisi ndio tutakuwa tunaanza safari nyingine mpya ya muziki. Sasa hivi kidogo tumesitisha mambo mengi ili tufanye hili jambo kwaajili ya taifa letu. Ninachowaambia mashabiki wetu wakae mkao wa kula kuna vitu vizuri vinakuja na watafurahia navyo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents