Habari

Makosa ya barabarani yaipatia serikali mamilioni ndani ya siku 4

Kaimu Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi, Lucas Mkondya, amesema ndani ya siku nne imekusanya shilingi milioni 410 Kwa makosa ya barabarani.

20161019_132300

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano hii jijini Dar es Salaam, Kamanda Mkondya alisema mapato hayo wameyapata kuanzia Oktoba 14 mpaka Oktoba 18.

“Jukumu letu kama jeshi la polisi ni kuhakikisha kuwa na usalama na sheria za usalama barabarani zinazingatiwa, hivyo basi kunakuwa na misako kila siku ya kuhakikisha kwamba wanaokiuka sheria barabarani wanapelekwa kwenye vyombo vya sheria hususan mahakama au wanatozwa faini zilizopo kisheria,” alisema.

“Kwahiyo kipindi hiki jeshi la polisi kanda maalumu tumeweza kukusanya jumla ya shilingi milioni 410 kupitia tozo ya makosa ya barabarani, kupitia kikosi cha kuzuia usalama barabarani imekamata makosa ya barabarani kuanzia Oktoba 14 mpaka Oktoba 18 na kuingizia serikali mapato hayo niliyokwisha yataja hapo juu,”aliongeza Mkondya.

Aidha kamanda huyo alisema idadi ya magari yaliyokamatwa yalikuwa 9,817, piki piki 708 na daladala 3268. Magari mengine binafsi pamoja na malori yalikuwa 6548 na kufanya jumla kuwa 10,525.

BY:EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents