Habari

Malkia Elizabeth kupata nyongeza ya mshahara

Malkia Elizabeth wa II wa Uingereza anatarajiwa kupata nyongeza ya mshahara kwa aslimiama 8 kutoka kwenye fedha za umma.

Nyongeza hiyo ni baada ya biashara ya ufalme kupata faida iliopanda kwa pauni milioni 24, uchukuaji wa marupurupu unatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya pauni milioni 6 kwa mwaka 2018/19.

Mnamo mwaka  jana akaunti ya fedha  ilionyesha kuwa matumizi kwa malkia  yalipanda kutoka pauni milioni 2 hadi kufikia pauni miolini 42. Aidha msimamizi wa fedha Alan Reid, ameeleza  kuwa Malkia aliwakilisha matumizi mazuri ya fedha.

Fedha anazopewa malkia na wizara ya fedha, zinatokana na faida ya biashara za malkia zilimpatia faida ya kiasi cha pauni milioni 24.7 hadi pauni milioni 328.8 kwa mwaka 2016/17 na zinashirikisha eneo kubwa la West End-Uingereza.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents