Habari

Mama anayemiliki nyumba moja ataharuki kudaiwa bili ya umeme ya tsh trilioni 637

Mwanamke mmoja kutoka jimbo la Pennsylvania nchini Marekani amejikuta katika hali ya taharuki baada ya kuletewa bili ya umeme kubwa kuliko hata gharama ya nyumba yake.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Mary Horomanski aliletewa bili ya umeme ya zaidi ya dola bilioni 284 ($284,460,000,000) za marekani ambazo sawa na Tsh Trilioni 637 baada ya kutumia umeme kwa miezi mitatu.

Bi. Mary Horomanski (58) amesema kuwa bili hiyo ilionyesha kuwa anatakiwa kulipa pesa zote ifikapo Novemba mwaka 2018 kitu ambacho kilimfanya aogope kuwasha taa na vitu vingine vya umeme siku ya Krismasi.

Sikuamini machoni mwangu baada ya kupewa bili yangu, kwani zilikuwa ni namba nyingi hadi nikashindwa kuelewa matumizi yangu ni ya kawaida na haijawahi kutokea hivyo, nashukuru wamenisaidia.“amesema Bi. Horomanski kwenye mahojiano yake na gazeti la Erie Times-News.

Hata hivyo baada ya kufuatilia kuhoji gharama hiyo ya bili, Kampuni ya umeme ya First Energy ilisema kuwa bili sahihi ilikuwa dola 284.46 na sio kama ilivyochapishwa awali na kukiri kuwa kulitokea hitilafu .

Msemaji Mkuu wa kampuni hiyo, Mark Durbin amesema kuwa hawakufahamu jinsi hitilafu hiyo ilivyotokea ikionyesha kuwa Bi Horomanski alihitajika kulipa $284,460,000,000 huku akitakiwa kulipa sehemu ya kwanza  dola 28,176 mwishoni mwa mwezi huu.

Sijawi kuona bili ya mabilioni ya pesa, nadhani ni makosa ya mitambo yetu kwani ni gharama kubwa sana kwa mtumiaji wa kawaida.” amesema Mark Durbin kwenye mahojiano yake na gazeti la Erie Times News.

Chanzo – Fire News Feed

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents