Michezo

Asante Kwasi wa Simba aanza mazoezi rasmi kuwavaa Ndanda

Hatimaye beki kisiki kutoka Lipuli FC, Asante Kwasi ameanza rasmi mazoezi na klabu yake mpya ya Simba SC.


Asante Kwasi akiwa na Mbaraka Yusuph wa Azam FC katika ufukwe wa Coco

Kwasi ambaye usajili wake uliteka vichwa vya habari, ameanza mazoezi na timu yake hiyo mpya leo asubuhi katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za ligi kuu na michuano ya kimataifa.

Simba inadaiwa kulipa kiasi cha shilingi milioni 35 kwa kumsajili beki huyo raia wa Ghana.

Timu hiyo ambayo inaoongoza msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara kwa pointi 23, siku ya Jumamosi itashuka uwanjani kupambana na Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents