Burudani

Ariana Grande na mpenzi wake Pete Davidson waonyesha jeuri ya fedha

Ariana Grande na mpenzi wake Pete Davidson ni mwendo wa kutumia pesa. Wapenzi hao wamehamia kwenye mjengo mpya wa kifahari ikiwa ni siku chache tangu waqanza mahusiano yao.

Couple hiyo mpya imedaiwa kuhamia kwenye jengo la apartment ya ghorofa ya kifahari iliyoundwa na mbunifu maarufu duniani Zaha Hadid ambayo ipo jirani na jengo la Manhattan’s Chelsea mjini New York.

Apartment hiyo ambayo wamehamia wawili hao inadaiwa kuwa na vyumba vitano vya kulala, mabafu manne na sehemu ya kufanyia mazoezi.

Hata hivyo bado haijafahamika kama Ariana Grande na Pete Davidson wamenunua mjengo huo au wamepanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents