Michezo

Man United, Real Madrid zagaragazwa na Barcelona kwenye rekodi hii kubwa barani Ulaya kwa msimu wa 2017-18

Man United, Real Madrid zagaragazwa na Barcelona kwenye rekodi hii kubwa barani Ulaya kwa msimu wa 2017-18

Tukiwa tunasubiria msimu mpya wa mwaka 2018-19 kwa sasa kuna rekodi mbalimbali za klabu kubwa duniani ambazo zinatolewa ambazo zimewekwa msimu uliopita wa 2017-18.

Kwa mwaka huu klabu ya Barcelona licha ya kushindwa kuchukua taji kubwa barani Ulaya lakini imetajwa kuwa ndio klabu iliyoongoza kutajwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii barani humo.

Barcelona kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram imetajwa mara bilioni 1.3 huku Real Madrid ikitajwa mara bilioni 1.02 na Manchester United inakuwa klabu ya tatu kuzungumziwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii ikitajwa mara milioni 782.

Takwimu hizo zilizotolewa na mtandao maarufu unajihusisha na masuala ya takwimu za kwenye mitandao ya kijamii wa  Blinkfire umezitaja klabu za Chelsea na Bayern Munich kushika nafasi ya nne na ya tano.

Sabau kubwa za Klabu ya Barcelona kuongozwa kutajwa imeeleza kuwa ni usajili wa wachezaji kama Coutinho, Yerry Mina, Dembele na kuondoka kwa Neymar, Mascherano na Andres Iniesta na kutwaa ndoo ya La Liga.

Kwa upande wa Real Madrid ni ubingwa Klabu Bingwa barani Ulaya na kupoteza mechi moja ya El-Clasico kumepelekea klabu hiyo kutajwa zaidi kwa msimu uliopita.

Kwa upande wa YouTube Barcelona imeongoza tena ambapo kuanzia mwezi Julai , 2017 hadi Juni 30, 2018 chaneli yao imeoneza views milioni 218 ikifuatiwa na mabigwa wa EPL Manchester City ambayo imepata views milioni 75.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents