Michezo

Haji Manara baada ya Simba SC kutoka sare na Waarabu ‘heshima ya nchi imelindwa’

Baada ya klabu ya Simba jana Jumatano Machi 07, 2018 kutoka sare ya goli 2-2 na klabu ya Al-Masry kutoka nchini Misri, Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amewashukuru mashabiki wote waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.

Haji Manara

Manara amesema kuwa kitendo hicho ni cha mashabiki ni cha kiungwana na kizalendo pia kinaleta heshima kwa taifa letu.

Kando ya Mwenyezimungu na wachezaji,hakuna anayestahili Shukran kama mashabiki mliokuja leo Taifa,mmetimiza wajibu wenu. Heshima ya nchi imelindwa🙏,“ameandika Manara kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Soma na Hii – Mvua yawaokoa waarabu, Mnyama Simba SC atoka na uchu

Mchezo wa jana Simba walionesha kiwango cha kutia matumaini kwa Watanzania ingawaje mchezo huo ulitawaliwa na mvua kali iliyoambatana na radi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents