Burudani

March 16: Afrika Mashariki yawakumbuka E-Sir na AK 47

Fahamu siku hii ya leo, March 16 ni siku ya kumbukumbu ya vifo vya waliokuwa wasanii E-Sir kutoka Kenya na msanii kutoka Leone Island Music Empire, Emmanuel Mayanja aliyejulikana kama AK 47.

E-Sir

Issah Mmari alikuwa ni mkali wa Hip hop kutoka Ogopa Deeays aliyeleta mapinduzi kwenye fani hii nchini Kenya kwa kasi miaka ya 2001-2003. Maisha ya dogo huyu yalipotezwa na ajali mbaya ya barabarani tarehe kama ya leo mwaka 2003 ambapo alikuwa kwenye gari moja na rafiki yake Nameless waliokuwa naye kwenye lebo moja (Ogopa deejays).

Pamoja na Nameless, walikuwa wakisafiri kutoka Nakuru wakirudi Nairobi baada ya kupiga show. Mwenzake Nameless alinusurika na majeraha kibao. Hadi kifo chake, E-Sir alikuwa na umri wa miaka 21 tu. Leo hii nyimbo zake kama vile ‘Boombatrain’ featuring Nameless, Mos Mos’, ‘Leo ni Leo’ na ‘Bamba’ featuring Big Pin bado zinaishi na milele zitazidi kupendwa kwa sababu bado tunampenda na ni kweli tunamiss vibe zake.

AK-47

Msanii huyu ambaye alikuwa ni mdogo wa msanii wa muziki kutoka Uganda Jose Chameleone alifariki akiwa na umri mdogo wa miaka 24, mwaka wa 2015 tarehe kama leo. Kifo chake kilitokea muda mfupi baada ya kukimbizwa hospitali.

AK k47 alikutwa akiwa amelala chini kwenye washrooms katika mojawapo ya clubs pande za Kampala. Utata mwingi ulizunguka kifo cha msanii huyu ambapo hakikubainika vizuri kwa wakati huo kilichopoteza maisha yake.

Imeandikwa na: Teddyza Agwa
@teddybway

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents