Michezo

Marcos Rojo atoboa siri ya goli lake, asema walifunzwa mbinu ya ushindi na Lionel Messi

Beki wa timu ya Taifa ya Argentina, Marcos Rojo amefunguka sababu zilizopelekea timu yake kushinda mchezo wa jana dhidi ya Nigeria kwenye michuano ya Kombe la Dunia huku akitupia goli pekee la ushindi.

Messi na Rojo wakishangilia goli la pili la ushindi

Rojo amesema wakati wakirudi mapumziko kipindi cha kwanza Lionel Messi aliwambia wachezaji wote wa Argentina kuwa haijalishi popote utakapokuwa kama utapata nafasi jaribu kufunga na sio kuwategemea washambuliaji pekee jukumu la kufunga.

Wakati tukiwa mapumziko ya kipindi cha kwanza, Messi alitwambia wote kuwa tunajukumu la kujaribu kufunga kwa nafasi zote tutakazozipata, yaani tulenge goli popote tutakapokuwa. Kwa hiyo nilivyoona mpira unakuja kwa upande wangu sikuwaza kingine zaidi ya kupiga golini na kweli mpira ukaingia.“amesema Rojo muda mfupi baada ya mchezo wa jana kumalizika.

Argentina wamefanikiwa kusonga mbele baada ya kuwachapa Nigeria goli 2-1 na watakutana na Ufaransa kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la dunia.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents