Michezo

Mario Mandzukic aipeleka Croatia fainali kombe la dunia

Timu ya taifa ya Croatia imefanikiwa kuingia hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuishushia kipigo cha mabao 2 – 1 Uingereza.

Mchezo huo uliyokwenda hadi dakika 120 baada ya kumalizika dakika 90 kwa sare ya 1 – 1 imemshuhudia mchezaji Mario Mandzukic akiibuka shujaa kwakuifungia bao la pili na la ushindi timu yake ya taifa ya Croatia.

Waliyotupia kwenye mchezo huo alikuwa mchezaji wa Uingereza, Trippier akifunga dakika ya tano tu ya kipindi cha kwanza kisha Croatia ikisawazisha kupitia kwa Perisic dakika ya 68 na  kuufanya mchezo huo kuwa mgumu baada ya kumalizika dakika 90 kwa sare hiyo ya 1 – 1.

Kisha kuongezwa dakika 30 na Mario Mandzukic akaipatia Croatia bao la pili dakika ya 109 na kuufanya mchezo huo kumalizika dakika 120 kwa ushindi wa mabao hayo 2 – 1.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents