Burudani

Mashabiki wa Future wamtisha mume wa Ciara

Katika kuadhimisha siku ya mama dunia hapo jana mume wa muimbaji Ciara, Russell Wilson, hakutaka kubaki nyuma na alitumia siku hiyo kueleza hisia zake juu ya mkewe na watoto wake.

Lakini mashabiki wa rapa Future walimjia juu Russ kwa kumwambia asijifanye yeye ni baba wa mtoto huyo. Russell aliandika haya “Hakuna kitu kizuri kama kuwa na wewe muda wote, wewe ni mama wa kipekee na pia ninafurahi kwa kuwa na wewe” kisha akaongeza “Nafurahi kuwa na wewe kwa maisha yangu yote na tuwalee watoto wetu. nakupenda sana.

Hapo ndipo mashabiki wa Future wakaanza kumporomoshea maneno kwa kumwambia anajifanya yeye ni baba bora kwa Future Jr. wakati mtoto huyo anae baba yake mzazi na sio yeye.

Hata hivyo mashabiki wa Russ hawakuwa mbali kujibu mashambulizi kutoka kwa mashabiki wa Future na wao wakaanza kumtetea Russell kuwa ni baba bora kwa mtoto huyo na kwa famila ya Ciara.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents