Habari

Matokea ya uchaguzi nchini Zimbabwe yazua Ghasia/ wanne wafariki

Matokea ya uchaguzi nchini Zimbabwe yazua Ghasia

Katika uchaguzi uliofanyika nchini Zimbabwe Ghasia zimezuka nchini humo kati ya wafuasi wa chama cha MDC dhidi ya vikosi vya usalama katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare,waandamanaji hao wakishinikiza kutangazwa kwa  matokeo ya uchaguzi nchini humo haraka.

Imeripotiwa kutokea kwa mauaji kwani watu wanne waliokuwa miongoni mwa waandamanaji ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Ingawa juhudi za kuwatawanya waandamanaji hao zikiendelea kwa tayari magari yenye maji ya washawasha tayari yameshaanza kazi ya kutawanya waandamanaji hao.

Ikidaiwa tangu alfajiri Makundi ya waandamanaji yalikuwa katikati ya mji mkuu Harare na ghasia zilizuka pale iliposikika kuwa chama cha Zanu Pf kimeshinda viti 110 kati ya viti 153 vya bunge na ikidaiwa matokeo ya Urais bado hayajawa tayari.

Hivyo wapinzani walivyosikia matokea hayo tayari wameona bwana Mnangagwa kaibuka mshindi ndipo wapinzani walipoanza kuchoma matairi na kuharibu alama za barabarani.

Maandamano hayo yanafanyika kuelekea katika ofisi za chama cha Zanu Pf huku waandamanaji hao wakibeba mawe wanaamini kwamba uchaguzi huo umekumbwa na udanganyifu wanataka mgombea wa MDC bwana Nelson Chamisa kutangazwa mshindi.

Kulingana na chombo cha habari cha ZBC Tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe Zec imetangaza kwamba Zanu Pf kufikia sasa imejishindia viti 110 huku MDC ikijipatia viti 41 tu.

 

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents