Burudani ya Michezo Live

Mazishi ya Kobe Bryant na binti yake Gianna ‘GiGi’ yafanyika kimya kimya, Tarehe ya kutoa heshima za mwisho yabakia pale pale mke wake athibitisha

Mazishi ya Kobe Bryant na binti yake Gianna 'GiGi' yafanyika kimya kimya, Tarehe ya kutoa heshima za mwisho yabakia pale pale mke wake athibitisha

Kobe Bryant na binti yake wa miaka 13, Gianna Bryant imeelezwa wamezikwa tayari. Kwa mujibu wa mtandao wa ET umeeleza kuwa mazishi ya wawili hao yamefanyika kwa siri sana katika eneo la Pacific View Memorial Park huko Corona Del Mar, California, siku ya Ijumaa, Februari 7, wiki mbili baada ya wao kufa katika ajali ya helikopta pamoja na wengine saba.

Nyota huyo wa zamani wa NBA yalihudhuriwa na mkewe, Vanessa Bryant, na watoto wake wengine watatu walioshiriki ambao ni, Natalia, 17, Bianka, 3, na Capri, miezi 7. “Vanessa na familia walitaka kufanya tukio hilo kwa siri huku chanzo kikiambia ET kuwa.

“Sherehe hiyo ya kumuaga ingekuwa ngumu sana kwa kila mtu kwani bado ni ngumu kwao kuamini kuwa wamepoteza watu wao wawili ambao wanawapenda sana.” Mbali na mazishi hayo ya siri, lakini akithibitisha kuwa sherehe za halaiki za kuwaaga Kobe na Gianna siku ya Jumatatu, Februari 24 katika ukumbi wa Staples Center huko Los Angeles, sehemu ambapo mchezaji huyo alicheza mpira wa kikapu akiwa na timu ya Los Angeles Lakers kwa kipindi chote cha miaka 20 ya kazi yake. February 24″ ni tarehe maalum, kwani ndio nambari ya Kobe aliyoitumia akicheza kwenye safari ya maisha yake tangu msimu wa 2006-07.

Vanessa alithibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa siku maalumu ya kumuaga Kobe Bryant na binti yake Gianna ni tarehe 24/2/2020 tarehe ambayo inaendana na namba ya jezi aliyoitumia wakati akicheza Los Angeles Lakers.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW