Mbowe afunguka kuhusu yeye na Wema Sepetu

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema clip ya sauti inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye na Wema Sepetu si ya kwake na hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mrembo huyo.

Wema na Mbowe

Kiongozi huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM, kuwa yeye anachukulia clip hiyo kama taarifa za kawaida za majitaka ambazo zinasambazwa wala hazina ukweli wowote.

“Kitu ambacho naweza kukisema kwa sasa hizo taarifa sio za kweli na timu yangu ya mtandao inajaribu kufuatilia kujua, na ukweli utajulikana muda sio mrefu,” amesema Mbowe.

Alipoulizwa kama anawajua waliofanya kitendo hicho, Mbowe amesema akizungumza sasa atakuwa anaharibu uchunguzi wao.

Pia ameongeza kuwa hajawahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Wema Sepetu kama inavyosikika kwenye clip hiyo ya sauti.

“Hapana yule ni kiongozi wa kijamii kwa maana kwamba ni mwanachama wetu aliyejiunga na chama chetu, na wapo wanawake, wasichana, wapo watu wengi kwenye chama chetu ni kwamba kuna mahusiano si kweli ni taarifa tu za upotoshaji,” ameeleza Mbowe.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW