Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Mbunge Mlinga afafanua hoja ya Diamond kujengewa sanamu

Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Mh Goodluck Mlinga amezidi kutetea hoja yake ya kuwa wasanii waliofanya vizuri na kuiwakilisha nchi nje vizuri, kupewa heshima kama kujengewa sanamu na baadhi ya mitaa na barabara kupewa majina yao.

Kipindi cha nyuma Mbunge huyo alisimama Bungeni na kusema kwa namna msanii Diamond Platnumz anavyoiwakilisha nchi vizuri kimataifa anastahili kujengewa sanamu, na kupendekeza ikibidi sanamu la askari posta Dar es Salaam liondolewe na kuweka hilo la Diamond.

“Na sikumtaja Diamond pekee, niliwataja wasanii wengi kama wakina Mr Nice ambao wameiwakilisha Tanzania sana nje lakini mpaka leo hii wamepotea hawana alama, inakuwa hawawezi kuwahamasisha wasanii wengine, lakini tunapoweka alama kila msanii anapofanya vizuri tunahamasisha wengine na ndiyo utaratibu katika nchi za wenzetu,” ameiambia Habari Xtra ya Times Fm na kuongeza.

“Kuna mchezaji mmoja wa mpira alitoka Kenya (Victor Wanyama) kuja Tanzania siku ya pili alipewa mtaa, sasa vile vitu ndio tunatakiwa tuvifanye kwa wasanii wetu wanaoibeba nchi. Sasa wewe fikiri mtu katoka nje ambaye anawakilisha nchi nyingine tunampa mtaa, lakini kwetu ni msanii gani alishawahi kuacha alama hata akapewa Barabara, hakuna!!!,” amemaliza kwa kusema.

By Peter Akaro

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW