Michezo

Mchezaji wa Hispania aliyepelekea timu yake kutolewa Kombe la Dunia aja Tanzania kupoza maumivu (+picha)

Ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu timu ya taifa ya Hispania kung’olewa kwenye michuano ya Kombe ya Kombe la Dunia na timu ya taifa ya Urusi tayari mastaa kibao wa timu hiyo wameanza mapumziko rasmi.

Image result for koke world cup penalty
Koke katikati kwenye picha (Picha na Getty Images)

 

Moja ya wachezaji hao ni Jorge Resurrección Merodio maarufu kwa jina la KOKE ambaye yeye wiki hii amewasili nchini Tanzania akitokea Hispania na kutembelea Hifadhi ya Taifa ya wanyama ya Ngorongoro.

Koke akiwa na mpenzi wake katika hifadhi ya Ngorongoro (picha kutoka kwenye ukurasa wake wa Instagram)

Koke (26) ni moja ya wachezaji wawili waliokosa penati zilizopekekea timu ya Hispania kutolewa kwenye Kombe la Dunia hatua ya 16 bora na timu ya taifa ya Urusi.

SOMA ZAIDI – Hispania wafuata nyayo za Ureno na Argentina kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents