Michezo

Mchezaji wa zamani wa Aston Villa, Thomas Hitzlsperger ajitangaza kuwa shoga

Mchezaji wa zamani wa klabu ya soka ya Aston Villa, Thomas Hitzlsperger amejitangaza kuwa ni shoga.

hitzlsperger-1er-footballeur-allemand-reveler-son-homosexualite

Mchezaji huyo mwenye miaka 31 aliyeshinda vikombe 52 na Ujerumani na aliyewahi kuzichezea pia West Ham na Everton, aliweka hadharani habari hiyo kwenye gazeti la Die Zeit. Hitzlsperger anakuwa mchezaji maarufu zaidi duniani kujitangaza hadharani kuwa ni shoga na amesema huu ni muda mzuri kufanya hivyo.

Kiungo hiyo aliyestaafu soka mwezi September mwaka jana amesema aligundua katika miaka michache iliyopita kuwa angependa kuishi pamoja na mwanaume na kuongeza kuwa: Sijawahi kujionea aibu kwa jinsi nilivyo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents