Michezo

Mchezo wa kamari ‘Betting’ wamtokea puani aliyekuwa mchezaji wa Man United Paul Scholes, akiuka sheria kwa kubet kwenye timu anayomiliki

Mchezaji Mstaafu wa Timu ya Taifa ya England na Klabu ya Manchester United, Paul Scholes atuhumiwa kwa kushiriki kubashiri(betting) matokeo ya michezo ya mpira wa miguu.


Kwa mujibu wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Uingereza(FA), Paul Scholes amejihusisha na ‘betting’ kwa kipindi cha miaka 4 hadi Januari mwaka huu.


FA imesema Scholes amekiuka kanuni za soka kwani alikuwa akifanya ubashiri huo hata wakati alipokuwa mmiliki mwenza wa timu ya Salford City.


Kwa muda wote huo Scholes alishiriki ‘betting’ mara 140 na endapo atakutwa na hatia atatozwa faini ya zaidi ya Tsh. Milioni 90.

Kwa mujibu wa The Gurdian. Msemaji wa FA alielezea tofauti iliyotumiwa sasa ni kama mtu ni mshiriki katika soka, maelezo yote yanayopangwa kuwa na wachezaji, mameneja, wamiliki, mawakala na yeyote anayefanya kazi ndani ya mchezo. “Utawala wa kidole ni kwamba ikiwa unafanya kazi katika soka huwezi kubet kwenye soka,” alisema msemaji huyo. “Haijalishi ikiwa ni bet kwenye klabu tofauti au nchi tofauti. Ikiwa wewe ni mshiriki katika soka, pesa zote zinazimwa. “

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents