Burudani

Mesen Selekta, Lulu Diva na Rubi walivyoandika historia Tigo Fiesta Mtwara (Picha)

Msanii Jerry Boniface maarufu kama Mesen Selekta akishirikiana na mdogo wake Gutta waliweza kuwapagawisha mashabiki kwa mtindo wao Singeli.

Msanii huyo alidhihirisha ubora wake uliopelekea uwanja kutimka vumbi kwa nyimbo zake za Kinanda, Kanyaboya, Dab Singeli.

Mji wa Mtwara ulikuwa tofauti na miji mingine kutokana na wasanii kuimba pamoja na mashabiki.

Akizungumza na waandishi wa habari Mesen Selekta alisema ” Hii inanipa mzuka kwa mashabiki kuukubali muziki wangu, nimeona jinsi shangwe la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote walivyolipokea wana Mtwara”.

Msanii mwingine aliyeiteka Mtwara alikuwa Farid Kubanda Fid Q aliwaamsha kwa wimbo wake Fresh, ambao aliurudia mara mbili kutokana na kiu ya mashabiki.

 

Kivutio kingine kilikuwa kwa MaDj Zero na Mafuvu waliweza kupiga mziki kwa zamu kama kwa kushindana hii iliweza kuleta ladha na Vibe la aina yake kwa mashabiki.

Kila Tamasha linapopita utafutwa msanii Chipukizi kupitia shindano la kusaka vipaji vya wasanii maarufu Kama Tigo Fiesta Supa Nyota, na kwa mkoa huo msanii, Siraji Mbuta kwa jina la kisanii Mbuta The Swagx aliibuka kidedea kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali mwezi ujao.

Kwa upande wa wadhamini Kampuni ya Tigo, Meneja wa Kanda ya Pwani, John Tungaraza alisema ‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+,’ Tungaraza alisema.

Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz.

Walioshusha vibe kama lote mjini Mtwara ni pamoja na kundi la Rostam (Roma and Stamina), Fid Q, Zaid na Weusii (Joh Makini, Niki wa Pili na G-Nako) ambao walikonga mioyo ya wapenzi wa muziki mjini Songea pia. Wengine ni wasanii wa bongo flava Mesen Selekta na Foby, wakongwe Chegge, Barnaba na Mr Blue, pamoja na akina dada Ruby na Lulu Diva.

TIketi za Tigo Fiesta 2018 – zitakuwa zinapatikana kupitia Tigo Pesa Masterpass QR kwa kupiga *150*01#, kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), na kuchagua namba 2 (lipa kwa Masterpass). Tuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents