Burudani

Mfahamu mtoto wa Jose Chameleon Abba Marcus anayefuata nyayo za baba yake

Mkongwe na daktari wa muziki wa dancehall Afrika kutoka nchini Uganda Jose Chameleon, anajivunia kitu ambacho wazazi wengi hutamani maishaini ambacho nikuwa na mtoto anayekuwa na vigezo kama vya kwake.

Dkt. Chameleon ambaye hupenda kuogelea mbali na kutengeneza muziki, anafurahia kukuza mtoto wake ambaye ni kifungua mimba kwa jina Abba Marcus aka T-rex ambaye ni rapper chipukizi na muogeleaji pia.

T-rex mwaka wa 2015, aliachia official video ya ngoma yake kwa jina Game Over aliyorekodiwa kwenye studio za babake, ambayo ilifanya vizuri nchini Uganda na kuwagusa mashabiki wa nguli wa muziki Afrika Jose Chameleon.

Mkali huyo wa Tubonge, amekuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha T-Rex anatimiza ndoto yake ya kuwa staa kama yeye. Na si tuu kimuziki bali hadi upande mwingine wa uogeleaji. Mwaka wa 2015, alidedea kidede katika mashindano ya uogeleaji ya watoto barani Africa akiwa pamoja na kakake Alpha Mayanja ambayo yalifanyika Jijini Nairobi Kenya.

T-rex tayari ameshawahi kuzipanda kumbi kubwa na kutumbuiza maelfu ya mashabiki wa muziki nchini Uganda, ikiwemo ni pamoja na show kubwa iliyopewa jina la #UgandaAllStars mwaka wa 2014.

Katika show hii Chameleon aliichukua fursa hiyo kumutambulisha T-rex kwa maelfu ya mashabiki wake kama rapper chipukizi kwenye ulingo wa muziki wa kizazi kipya. Jose Chameleon anajiunga na mastaa wengine duniani kama vile Willy Smith mwigizaji mwenye haiba ya juu nchini Marekeni na dunia akiwa anakula matunda ya ufanisi kutoka kwa mtoto wake Jaden Smith ambaye toka kuzaliwa kwake amekuwa akiigiza kwenye filamu pamoja na babake.

Burudika na video ya awali inayoonyesha show ya UgandaAllStars ambapo Chameleon alimpandisha jukwaani mtoto wake rapper chipukizi T-rex.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter @ : ChangezN
Instagram: changez_ndzai

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents