Mfahamu Timaya ambaye anajipanga kuachia albamu ya GRATITUDE

Anaitwa Inetimi Timaya Odon kwa jina lake la kuzaliwa kabisa lakini kwenye jina la sanaa anatumia jina la “@timayatimaya ”

Timaya alizaliwa mwaka 1980 huko nchini Nigeria.

Kwenye sanaa @timayatimaya alianza rasmi mwaka 2005 na ngoma yake ya kwanza kabisa ilikuwa inaitwa “DEM MAMA”

Baada ya hapo aliendelea kutoa kazi mfululizo na alifanikiwa kuachia Album yake ya kwanza ambayo aliipa jina la ”TRUE STORY”

Baada ya hapo aliendelea kutoa album zingine kama Gift and Grace,De Rebirth,Epiphany,Llnp,Upgrade na zingine nyingi.

Mpaka sasa Timaya ameweza kushirikiana na wasanii wengi sana kwenye kazi zake Kama Patoranking,Burnaboy,Sean Paul,Phyno na wengine wengi.

Mwaka 2019 Timaya alijizolea mashabiki wengi sana hapa Tanzania hasa baada ya kutoa EP yake ijulikanayo kama “CHULO VIBES” na ndani ya Ep hiyo alimshirikisha msanii mkubwa sana hapa Tanzania Ali Kiba kwenye ngoma ambayo ilipewa jina la “Number One” na ngoma hiyo ilimpatia mashabiki wengi sana kutoka hapa Tanzania.

Mwaka huu 2020 akiwa amekaa miaka 6 bila kutoa Album yoyote na akiwa anatimiza miaka 15 toka ameanza kazi ya muziki hatimaye ameamua kutoa zawadi ya Album kwa mashabiki zake na Album hiyo ameipa jina la “GRATITUDE”

Kwenye baadhi ya mahojiano yako amesema sababu kubwa ya kutoa Album hii na kuipa jina la “GRATITUDE” ambapo kwa kiswahili ina maanisha “SHUKRANI” ni sehemu ya yeye kushukuru kwa Mungu pamoja na mashabiki wake kwa mafanikio ambayo ameyapata katika kipindi ambacho ameanza sanaa mpaka leo ambapo anatimiza miaka 15 kwenye kazi ya muziki.

Kwenye Album hii ya TIMAYA imesheheni nyimbo kali sana na zenye ujumbe wa mkubwa Kama vile Gragra,I can’t kill myself,The Mood,Born to Win,No limit,The Light na zingine nyingi ambazo zinapatikana kwenye Album hii.

Hii ni Album ambayo mapokezi yake yamekuwa makubwa sana.

Kwa Sasa Album hii ya “GRATITUDE” inapatikana kwenye digital platform zote kwa Sasa lakini pia video ya ngoma ya moja ya Album ya GRATITUDE ijulikanayo kama Gragra imetoka na mapokezi yake yamekuwa makubwa sana kwenye mtandao wa youtube.

Album hii ya #GRATITUDE kutoka kwa @timayatimaya kwa Sasa inapatikana kwenye digital platform zote du

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW