Habari

Mh. Zitto aachiwa, polisi wachukua simu yake

Kiongozi wa Chama chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe ameripoti kituo cha polisi kilichopo Kamata Karikakoo jijini Dar es salaam kama alivyotakiwa na jeshi hilo. Jeshi hilo limechukua simu ya Mh. Zitto kwa maelezo kuwa itasaidia uchunguzi wao.

Katibu – Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Ado Shaibu amesema kuwa baada ya kuichukua simu hiyo wameahidi watairudisha kwake kesho jioni huku akitakiwa kuripoti kituoni hapo Novemba 27 mwaka huu.

Pia ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa litakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha ACT – Wazalendo, kwa Lengo la kufanya upekuzi wa Ofisi hizo wakitafuta nyaraka zilizotumika na Chama kufanya uchambuzi wa takwimu za Serikali ambao unaonyesha uchumi wa nchi yetu unasinyaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents