Habari

Mh. Zitto awakingia kifua wakulima wa Maharagwe

Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa ukosefu wa barabara ya Kigoma – Nyakanazi umewafukarisha Wananchi hawa na kusababisha soko la mazao yao kuwa duni.

Zitto ambaye yuko ziarani kutembelea Kata zinazoongwa na Chama hicho ameeleza kuwa wakulima wa maharagwe Katika Kata ya Biturana, Halmashauri ya wilaya Kibondo wanauza maharage yao ya njano kwa shilingi 700 – 800 kwa kilo moja,lakini maharage hayo hayo yakifika Dar es salaam na miji mingine mikubwa yanauzwa 1800 – 2000 kwa kilo.

Wakulima wa Maharagwe Katika Kata ya Biturana, Halmashauri ya Wilaya Kibondo wanauza maharage yao ya njano kwa shilingi 700 – 800 kwa kilo moja. Lakini Maharage hayo hayo yakifika Dar na miji mingine mikubwa yanauzwa 1800 – 2000 kwa kilo. Ukosefu wa barabara ya Kigoma – Nyakanazi umewafukarisha Wananchi hawa na kusababisha soko la mazao yao kuwa duni.

Kata hii yenye wakazi 12,000, pia inapakana na kambi ya wakimbizi ya Nduta, lakini watu wa Biturana hawana Maji ya kunywa ilhali wakimbizi wana huduma ya maji safi na salama. Kuna haja kubwa ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuhakikisha vijiji vinavyopakana na kambi za wakimbizi vinapata huduma muhimu kama Maji, ili kutosababisha wananchi kuwa na chuki na wakimbizi.

Inasemwa Kigoma ni Mkoa Masikini kuliko yote. Umasikini huu unatokana na KUFUKARISHWA kwa kukosa miundombinu ya barabara nk. Ni kielelezo cha uwiano hasi kati ya maendeleo vijijini (wanakozalisha) dhidi ya maeneo ya mjini, ACT Wazalendo tumelieleza kwa upana hili kwenye Azimio la Tabora.

Jana ziara ya Viongozi wa ACT Wazalendo ilitembelea Kata ya Biturana, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo. Diwani wetu wa hapa, ndugu Barnabas Baranzila amejaribu kutatua changamoto hizi, amehamasisha wananchi wake, na kwa pamoja wamechonga barabara kutoka kwenye vijiji vya Kata hii mpaka hapa makao makuu ya Kata, Birurana, lengo ni kurahisisha usafirishaji wa mazao yao, na hivyo kupunguza unyonyaji kwenye soko la mazao yao. Kazi yake ya karibuni ni uchongaji wa barabara uliofanywa na wananchi wenyewe kutoka katika Kijiji cha Nengo mpaka hapa Biturana.

Sisi ACT Taifa tutawasaidia kuunda ushirika imara wa wakulima wao ili kuhakikisha hawanyonywi katika soko la mazao yao, na tutawasaidia kusemea suala la maji kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa, hasa yanayojihusisha na masuala ya wakimbizi.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Kata ya Msambara
Kasulu Mjini
Machi 6, 2018

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents