Habari

Mifupa ya binadamu yaokotwa

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule amethibitisha kuokotwa kwa viungo vya mwili wa binadamu katika bwawa la maji la Jomu wakati watu wakitafuta maji, Tinde mkoani Shinyanga.

Kamanda Haule akiongea na waandishi wa habari alidai kuwa siku ya Jumatatu watu walipoona viungo hivyo walitoa taarifa kwa jeshi la polisi.

“Fuvu la kichwa limepatikana hapo bwawani, taya ya binadamu, lakini hizi hapa ni mbavu za binadamu 14. Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo jeshi la polisi lilichukua hatua za haraka kufika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa awali tukishirikiana na daktari mtaalam wa viungo vya binadamu katika tukio hilo mifupa inayosadikiwa ni ya binadamu katika bwawa hilo ni pamoja na fuvu la kichwa, eneo la mguu sehemu ya paja,mifupa miwili ya mkono, mfupa mmoja wa mguu sehemu ya goti mfupa mmoja wa sehemu ya bega na mifupa 14 mbavu ,” alieleza Kamanda Haule.

Kamanda Haule alielezaa kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ikiwa pamoja na kufungasha mifupa yote na kupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kufanya vipimo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents