Burudani

Mike Tee afungua kampuni itakayotangaza nyimbo za wasanii na kuziuza

Rapper mkongwe, Mike Tee aka ‘Mnyalu’ amesema aliingia kufanya muziki ili apate connection za watu tu na sio pesa ambapo kwasasa amefungua kampuni ya kutangaza nyimbo za wasanii pamoja na kuziuza.

mike-tee

Akizungumza na Bongo5 leo, Mnyalu amesema mfumo wa kutangaza na kuuza nyimbo za wasanii kwa njia ya mtandaoni chini ya kampuni yake utaanza February mwaka huu.

“Nimekuwa nikifanya maandalizi na research ya utaratibu wa kuuza nyimbo na kutangaza kwa mwaka mmoja ambapo kwasasa nimefanikiwa. Utaratibu huu ulikuwa uanze kutumika kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu ila kuna mambo ambayo yalikuwa hayajakamili ila tunategemea mwezi ujao utaanza,” amesema.

“Kitu kimoja ambacho nilikiangalia kwanini biashara ya single hapa kwetu haifanyiki nikafanya research nikaona nitengeneze kwanza mfumo ambao kwasasa umemalizika. Kwahiyo tutaingia mkataba na msanii wa kusambaza nyimbo na kuiuza. Kwahiyo biashara ya nyimbo itakuwa na manufaa kwa wasanii.”

Rapper huyo amesema ameamua kufanya shughuli zake nyingine na harakati za muziki kuzipa kisogo kwanza.

“Kuna kitu kimoja ambacho wanasema lazima uchague kitu kimoja ambacho utakifanya vizuri zaidi kuliko kufanya kila kitu. Mimi nilikuwa nimeajiriwa, nimefanya kazi kwenye makampuni ya mawasiliano kama miaka 7,kwahiyo kwasasa hivi nipo kwenye hiyo kampuni ambayo tumeianzisha.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents