Burudani

Mke wa Roma adai alikata tamaa kumpata mume wake

Jumapili hii, Aprili 23 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya mke wa rapa Roma Mkatoliki, Nancy ambapo alipata fursa ya kusherekea siku yake hiyo muhimu akiwa na mume wake, ambaye bado anauguza majeraha aliyoyapata baada ya kutekwa na watu wasiojulikana na baadaye kuachiwa.

Nancy akimlisha keki mume wake, Roma.

Nancy alikuwa mmoja kati ya watu walioweza kupambana huku na kule, ndani ya siku 4, kutafuta taarifa zilizosaidia kupatikana kwa mume wake huyo ambaye alitekwa pamoja na watu wengine watatu.

Jumapili hii baada ya kusherekea siku yake muhimu ya kuzaliwa akiwa na mume wake, amedai alikata tamaa kama angepata nafasi ya kusherekea siku hiyo muhimu na mume wake tena.

“lifika wakati nilikata tamaa na kuamini kuwa sitakuwa na wewe katika sikukuu ya kumbukumbu yangu ya kuzaliwa ya mwaka huu!! Lakini Mungu Baba Wa Mbinguni akasema no. #MyBirthday2017,” aliandika Nancy Instagram.

Roma na wezake watatu walitekwa na watu wasiojulikana wakiwa Tongwe Records, Masaki Jijini Dar es salaam, ambapo mpaka sasa jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents