Burudani

Moni amtuhumu Roma Mkatoliki kuwageuka

Msanii wa muziki Moni Centrozone, aliyewahi kutekwa akiwa na Roma Mkatoliki na Bin Laden, katika studio za Tongwe amemjia juu Roma kwa kutoboa siri ya utekwaji na kujiongelea yeye.

Moni amesema hayo kupitia Enewz ya EATV, na kumtuhumu mkali huyo kutumia ngoma ya ‘Zimbabwe’ kuelezea utekwajwi na kujisimulia peke yake kama alikuwa ametekwa mwenyewe.

“Unaua kwanza ishu iliyojitokeza imekaa katika nasfi ya kwanza umoja, mtu anajiongelea yeye mwenyewe kwenye hiyo ishu as if alikuwa kwenye matatizo peke yake kwa hiyo ishu ni kwa manufaa yake,” amesema msanii huyo.

Akaongeza kuwa “Mimi naangalia maisha yangu na muziki na sitaki kuongea habari za mtu mwingine, wala sijaongelewa mtu yeye kajiongelea kama yeye kwamba alitekwa nini kwa manufaa yake yeye kama yeye.”

“Naweza kuamua na mimi nikatoa dude lolote ambalo litanizungumzia mimi peke yangu na maisha yangu jinsi nilivyotekwa, kwa sababu kuna matukio ambayo na mimi nayakumbuka,” alisisitiza Moni.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents