Habari

Mr Nice azingua tena, awadanganya wanahabari Kenya kwamba hakuwa na mkataba na meneja wa Tanzania

Hitmaker wa Kidali Po, Nice Mkenda aka Mr Nice leo anadaiwa kudanganya mbele ya jopo kubwa la waandishi wa habari alipokuwa akisaini mkataba mpya na Candy n Candy Records ya nchini Kenya. Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa Kenya, Ghafla, Mr Nice anadai kuwa mkataba wa awali kabla ya kwenda Grandpa Records ulikuwa unaisha baada ya miezi 6 ya kutofanyika project yeyote.

547858_531795850196323_2038515980_n

Mtandao huo umepata nakala za mkataba wa miaka mitano aliosaini na Watanzania, Sallam Ahmed Sharaff na Ramadhani Juma Fataki ambaye anafahamika zaidi kama Lamar, producer wa Fish Crub uliosainiwa February 2, 2012 – February 1 2017 ambapo kama pande yoyote ikivunja mkataba huo itatakiwa kulipa shilingi milioni 50.

Bongo5 imezungumza exclusively na Sallam Ahmed Sharaff ambaye ni anasomeka kama Meneja wa kwanza kwenye mkataba huo, anayesema bado wana mkataba na Mr Nice na mikataba yote anayosaini kwa sasa ni hewa.

“Mimi sijavunja mkataba naye,” amesema. Kwahiyo nikisema namwachia yeye atanidai mimi milioni 50 kwahiyo hapo ntakuwa nimevunja mkataba wangu, mimi nasema sijamwachia bado, yeye kama kasaini kasaini hewa.”

“Siku atakayoanza kuperform tutapanda kwenye sehemu ya show na kuchukua mapato yetu tusilaumiwe na mtu,” ameongeza.

“Albam yake ipo tayari kwa Lamar, yeye katoroka tu. Mkataba wenyewe uliooneshwa unajieleza, Wakenya wenyewe wataelewa, kwahiyo hao Candy watafuta nani Lamar, watanitafuta mimi, itabidi wakae chini waongee. Kama hawawezi kuongea, sisi tutaendelea na shughuli yetu, siku yeyote tunaweza tukatoa wimbo wa Nice ambao umehit sisi tunauchukua tunautengenezea ringtone tunachukua hela yetu wala hatuna tatizo”

Hizi ni nakala za mkataba huo.

slide-1-638

slide-2-638

slide-3-638

slide-4-638

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents