Habari

Msanii wa Filamu Shamsa Ford apost picha ikimuonyesha na majeraha usoni,maneno yake yaonyesha kupigwa na mume wake

Msanii wa Filamu Shamsa Ford apost picha ikimuonyesha na majeraha usoni,maneno yake yaonyesha kupigwa na mume wake

Star wa Filamu Hapa Nchini Shamsaford ameamua kutoa yaliyo Moyoni kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram na kuelezea jinsi anakerwa na tabia za Wanaume ambao wanawanyanyasa Wake zao ambao walifunga nao Ndoa.

Kauli hiyo ya Shamsa imeambatana na picha yake Ikimuonesha akiwa na alama usoni ya Kupigwa Pembeni ya Jicho la Kushoto na kuandika hivi

” wanawake ambao tuna mapenzi ya dhati ndo huwa tunaonewa sana.Wanawake ambao huwa tunaishi maisha ya uhalisia kutokana na mifuko ya wanaume zetu ndo tunaonewa na kuonekana washamba.Lakini wale wanawake wachunaji ndo huwa wanapewa kipaumbele na kuthaminiwa .Sielewi wanaume huwa wanataka nn kutoka kwa wanawake.Tunapigwa,tunasemwa vibaya,tunaonewa ,tunabeba mizigo mikubwa lakini mwisho wa siku bado unafuta machozi na kusema ALHAMDULILAH .Nyie wanaume huwa mnataka nini?🙌🙌 …”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents