Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Mtanzania aliyewahi kufanya kazi kwa Bill Gate aeleza mazito kuhusu tajiri huyo

Kijana Benjamin Fernandes ambaye aliwahi kufanya kazi kwa tajiri namba moja wa dunia Bill Gate, amefunguka juu ya furaha yake ya kumuona mtu huyo Tanzania.

Kupitia mtandao wa Instagram Benjamini ameandika kuonyesha furaha ya kukutana na mtu huyo ambaye ametua nchini kwa siku kadhaa na kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Tanga na kisha kukutana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Mwaka mmoja uliopita, nilikutana na Bill Gates kwa mara ya kwanza nilivyokuwa nikifanya kazi katika shirika la Bill and Melinda @gatesfoundation . Nakumbuka kua na woga lakini nikamwambia nimetoka Tanzania aliponiuliza juu ya fulana yangu imetokea wapi na nikamkaribisha nchini kwetu. Mwaka mmoja umepita na leo nimekutana na Bill Gates tena hapa nchini kwetu #Tanzania. Navutiwa sana na Bill Gates kwa jinsi anavyojitoa katika kusaidia na kuinua watu waliomzunguka na dunia nzima kwa ujumla. Maisha ya kila mmoja yana thamani sawa; kitu ambacho Bill Gates amekua akionyesha mfano katika kazi zake. // One year ago, I met Bill Gates for the first time when I was working for the Bill and Melinda Gates Foundation. I remember being so nervous. I told him that I was from Tanzania when he asked where my shirt was from. I told him he should come to Tanzania soon. Today, one year later. I meet Bill Gates again, here in my home country of Tanzania. I admire this man so much and how much he commits to supporting people around him in the world. All lives have equal value. Something we see Bill and the foundation exemplify in their work
#TanzaniaKwanza #BillGates#DarEsSalaam #Tanzania

ameandika kijana huyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW