Burudani

MTVMAMA: Diamond ashinda Best Live Act, Wanaijeria wazitawala

Diamond Platnumz ndio mtumbuizaji bora barani Afrika. Hitmaker huyo wa Nana jana alishinda tuzo ya Best Live Act kwenye MTV MAMA Awards zilizotolewa jijini Durban, Afrika Kusini.

11252563_873456646067687_909310217_n
Diamond akiwa na meneja wake, Babu Tale baada ya kuchukua tuzo

Muimbaji huyo ambaye pia alidondosha show ya kukata na shoka kwenye tuzo hizo akiwa na msanii wa Nigeria, Flavour na kuimba hit yao, Nana, amewashukuru watanzania na wengine waliomwezesha kushinda tuzo hiyo.

“Shukran Kubwa sana Zimfikie Mwenyez Mungu kwa Tuzo hii, na pia Shukran za Dhati Ziwafikie Wadau, Media, Wasanii na Mashabiki zangu wote #TeamWasafi kwa kunipigia kura na Kuhamasisha kwa Nguvu,” ameandika kwenye Instagram.

“Niushkuru sana Uongozi wangu, Familia pamoja na Team nzima ya @wcb_wasafi hususan Madancers wangu kwani Naamini wao ndio wamenipika nikapikika hadi leo hii kuweza kuletaTunzo hii Nzito ya Mtumbwizaji Bora Africa, Nyumbani…lakini pia Shukrani za kipekee zimfikie Mama yangu kipenzi Sandra kwa Mafunzo na Malezi anayonipa kila siku juu ya Dunia,” ameongeza.

“Na Shukran tena za kipekee na aina yake zimfikie Roho yangu, Kipenzi Changu @zarithebosslady Kwa raha na Usingizi mwanana anipatiao na kunifanya nizidi kutunga na kuwa M’bunifu kwenye kazi..emoji #BestLiveAct #Mtvmama2015 Asanteni sana.”

11199470_1002922379731138_968098397_n

Hata hivyo ni wasanii wa Nigeria ndio waliotawala tuzo hizo huku P-Square wakiondoka na tuzo mbili.

Hii ni orodha nzima

Best Female: Yemi Alade (Nigeria)
Best Male: Davido (Nigeria)
Best Group: P-Square (Nigeria)
Best New Act Transformed by Absolut: Patoranking (Nigeria)
Best Hip Hop: Cassper Nyovest (South Africa)
Best Collaboration : AKA, Burna Boy, Da LES & JR: “All Eyes On Me” (SA/Nigeria)
Song of the Year: Mavins: “Dorobucci” (Nigeria)
Best Live: Diamond Platnumz (Tanzania)
Video of the Year: “Nafukwa” – Riky Rick; Director: Adriaan Louw Best Pop & Alternative: Jeremy Loops (South Africa)
Best Francophone: DJ Arafat (Ivory Coast)
Best Lusophone: Ary (Angola)
Personality of the Year: Trevor Noah (South Africa) MAMA Evolution: D’Banj (Nigeria)
Best International: Nicki Minaj Artist of the Decade: P-Square MTV Base Leadership Award: Saran Kaba Jones & S’Bu Mavundla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents