Burudani

Muendelezo wa Straight Outta Compton unakuja, kuangalia maisha ya Snoop Dogg, Tupac na Nate Dogg

Filamu Straight Outta Compton iliyoangaza maisha ya kundi la N.W.A. lililoundwa na Dr Dre, Ice Cube, Eazy E na wengine iliingiza zaidi ya dola milioni 56 kwenye wiki yake ya kwanza ndio maana imewapa moyo watayarishaji kutengeneza muendelezo wake.

0820-snoop-and-crew-getty-composite-7

Kwa mujibu wa TMZ, flamu nyingine itakuja itakayoangalia maisha ya Snoop Dogg, Tupac na rappers wengine wa West Coast.

Rapper wa Dogg Pound, Daz Dillinger ameuambia mtandao huo kuwa filamu hiyo itaanzia pale N.W.A. ilipoishia na kuangalia maisha ya Snoop, Nate Dogg, Kurupt, Daz na Warren G. Filamu hiyo itaitwa ‘Dogg Pound 4 Life.’

Inadaiwa kuwa mtoto wa Dr. Dre, Curtis Young, ataigiza nafasi ya baba yake. Bado hakuna mtu aliyefahamika atakayemuigiza Snoop na Ice Cube japo waigizaji hao hawatakuwa wale wale waliogiza kwenye filamu ya ‘Compton.’

Dre na Cube hawataitayarisha filamu hiyo lakini Daz anadai kuwa Cube ameibariki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents