Habari

Mugabe kuhamishia makao makuu ya Zimbabwe katika wilaya anayotoka

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe yupo kwenye kitimoto baada ya serikali yake kuwa na mipango ya kuhamisha mji mkuu kutoka Harare hadi kwenye wilaya anayotokea, mpango ambao viongozi wa upinzani wanasema hawakushirikishwa.

Waziri wa serikali za mitaa Ignatius Chombo wiki hii alidai kuwa mipango inaendelea kujenga jengo jipya la bunge, ofisi za serikali, ikulu na nyumba za kukaa huko Mt Hampden, takriban kilomita 40 magharibi mwa Harare ili uwe mji mkuu mpya.

Bwana Chombo alisema uamuzi huo ni kupunguza mlundikano wa watu jijini Harare ambako kuna zaidi ya watu milioni 1.6.

Jiji lililopendekezwa ni katika wilaya ya Zvimba ambayo ni wilaya ya Mugabe na pia hupata fedha zaidi za maendeleo kutoka serikali licha ya kuwa na wakazi wachache.

Makampuni ya kichina ambayo huhusika na uchimbaji almasi na ambayo yamewekeza kwenye mahoteli na shopping malls nchini humo yanatarajiwa kupewa ukandarasi wa mradi huo mpya.

Wananchi wengi wa Zimbabwe wanahoji mantiki ya kujenga jiji jipya wakati maeneo mengi ya mjini yanadorora kutokana na matatizo ya kiuchumi yaliyodumu kwa kipindi kirefu.

Wilaya ya Zvimba tayari inaongoza kwa kuwa na barabara bora nchini humo na makazi mengi yana umeme.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents