Muigizaji Elizabeth ‘Lulu’ Michael aanza kutumikia kifungo cha nje, hili ndio eneo alilopangiwa

Muigizaji wa filamu nchini, Elizabeth ‘Lulu’ Michael ameanza kutumikia kifungo  chake cha nje leo Mei 15, 2018 kama moja ya masharti aliyopewa baada ya kuachiwa kutoka gerezani jana.

Related image

Lulu akiwa na wenzake 10 wamepangiwa kufanya usafi katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani zilizopo Posta Jiji la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka  Mkurugenzi wa Probesheni na Huduma za jamii, Charles Nsanze amesema kila siku mwigizaji huyo atatumia saa nne kusafisha mazingira kisha ataendelea na shughuli zake nyingine za ujenzi wa taifa.

Atapumzika siku za Jumamosi na Jumapili au siku za sikukuu, hatakuwa peke yake kwa kuwa tayari hapa wapo wafungwa wengine tisa wanaofanya kazi za usafi wa mazingira.” amesema Nsanze kwenye mahojiano yake na gazeti la Mwananchi.

Soma zaidi hapa – Lulu aachiwa huru, kutumikia kifungo cha nje

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW