Lulu aachiwa huru, kutumikia kifungo cha nje
Msanii wa Maigizo, Elizabeth Michael(Lulu) amebadilishiwa kifungo na sasa anatumikia adhabu hiyo anatumikia akiwa nje.
Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba 13 mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.
Akizungumza na MCL, Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
“Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, kitaalamu tunaita ‘community service’” amesema Mboje.
Kesi ya Lulu ilikuwa ikisikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Ikiongozwa na Jaji Sam Rumanyika.