DStv Inogilee!

Muigizaji wa Nollywood aeleza kwanini ndoa yake imevunjika na funzo kwetu sisi

Muigizaji wa Nollywood, Ini Edo ameamua kueleza runinga nchini humo sababu za kuvunjika kwa ndoa yake ya miaka mitano na Phillip Ehiagwina wa Marekani.

Ini-Edo-1

Muigizaji huyo asiyependa mambo yake yaongelewe sana kwenye mitandao na vyombo vya habari, aliweza kuelezea kwa uwazi mambo anayodhani yalisababisha ndoa yake ya miaka mitano kuvunjika.

Ndoa yake ambayo anasema kwa kiasi kikubwa iliathiriwa na umbali kwakuwa mumewe alikuwa Marekani yeye yupo Naijeria hivyo ukiondoa matatizo waliyokuwa nayo lakini wangekuwa wanakaa pamoja muda mwingi ilikuwa rahisi kushughulikia tofauti zao. Anasema umbali huo ulifanya mambo yakawa magumu zaidi.

Ingawa kulikuwa na tetesi kwamba aliamua kuchagua kazi yake ya uigizaji na kuachana na mambo ya familia, yeye anasema hivi kwenye mahojiano hayo:

Niliamua kuolewa  kwasababu nilikuwa nahitaji kuwa na familia, na sifikirii kwamba kuna mtu atasema kwamba napenda sana taaluma yangu zaidi ya familia ingawa taaluma yangu ni muhimu pia.!

Ukimuuliza hasa ni sababu gani iliyosababisha ndoa hiyo kuvunjika, hana sababu ya moja kwa moja  ila anachoweza kusema ni kwamba, ” Kwa hakika hatukuwa na sababu ya moja kwa moja. Unajua haya mambo yanavyokwenda narudia kama nilivyosema kwamba hatuendani kabisa na mara nyingine kuna baadhi ya vitu tulishindwa kufikia muafaka wake na mambo mengine kushindwa kuwa na msingi mmoja hivyo tukashindwa kwenda pamoja”

Alipoulizwa kama aliingia kwenye ndoa mapema alisema, “Sifikirii kwamba ilikuwa mapema sana, umri wangu ulikuwa unatosha kabisa ila nilikuwa na haraka kidog.”

Na alipoulizwa kama filamu zake zimeathiri ndoa yake pia aliendelea kusema, ” Nimejitahiji kujiheshimu sana hasa nilipoingia kwenye ndoa. Na ni kweli kuna sehemu ambazo huwezi kuigiza unapokuwa umeolewa.”

Kitu kingine cha msingi alisema kutokana na umaarufu wao wa kuonekana kwenye TV wanawavutia watu wengi na wengine ambao si sahihi. Hivyo hujikuta wakifuatwa na watu wa aina mbali mbali na watu hawa hushindwa kutofautisha maisha ya kuigiza kwenye filamu na maisha halisi.

Ukweli ni kwamba kama ni msichana ni yule yule si kwamba kwasababu wao wanaonekana kwenye TV basi ni wa tofauti, hapana wote ni binadamu wa kawaida hivyo kwenye TV ile ni taaluma lakini maisha ni sawa na mtu mwingine yeyote.

Alipoulizwa kama anajuta kuingia kwenye ndoa hiyo anasema kamwe hatajuta  ila kuna uzoefu alioupata na kuna vitu vya kijifunza.

Kuachana huko kumemfanya awe jasiri, na kumfanya akomae kifikra.

“Hivyo siwezi kusema ninajutia kila kitu, nimejifunza somo langu.”

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW