Burudani

Muziki wa sasa ni kama vita – Darassa

Rapper Darassa amesema muziki wa sasa si rahisi tena na umegeuka kuwa kama vita.

10982135_861873537207718_5235137461212258573_n

Darassa ambaye ndani ya mwaka huu tayari ameshaachia nyimbo mbili, Tunaishi na Cinderella, ameiambia Bongo5 kuwa, anatarajia kuja na wimbo ngoma mpya iitwayo ‘No Retreat No Surrender’.

“Kitu ambacho kipo kwenye kichwa changu ni kuandaa project nyingine ambayo itatoka baada ya video ya Cinderella kutoka mwezi huu unaoanza. Project ambayo naiandaa baada ya kazi hiyo nitakuja na ngoma ‘No retreat no surrender,” amesema.

“Unajua huu muziki umeshakuwa vita sasa hivi, Sio kazi kama ambavyo watu wanaongea wala sio mchezo kama ambavyo unavyoweza kuita ni game. Hii ni game ambayo imekuwa tofauti na game tuliyokuwa tunaielezea mwanzo. Hii ni ya hatari zaidi, unatakiwa kuonesha kile ulichokuwa nacho au kutumia ulichokuwa nacho ili uendelee kuishi. Kwa sababu hata mwanzo niliwahi kuzungumzia changamoto nilizopitia, kwahiyo sasa hivi ni kikamanda zaidi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents