Habari

Mwalimu afukuzwa kazi baada ya kuwaambia wanafunzi ‘Father Christmas hayupo ulimwenguni’

Mwalimu mmoja amepoteza kazi baada ya kuwaambia wanafunzi wake kuwa Santa Claus ama maarufu kama Father Christmas hayupo ulimwenguni.

Mwalimu huyo msaidizi alikuwa akifundisha wanafunzi wa darasa la kwanza huko New Jearsey nchini Marekani.

Santa Claus ama Santa kwa ufupi ni hekaya ya zamani ambayo yadaiwa babu huyo mwenye ndevu nyeupe zinazofika tumboni na ambaye juvalia mavazi ya rangi nyeupe na nyekundu pamoja na kofia huwapatia zawadi watoto watiifu katika mkesha na asubuhi ya siku ya Krismasi.

Hekaya hiyo maarufu sana katika nchi za magharibi na huaminiwa kabisa na watoto.

Mwalimu huyo pia inadaiwa aliwaambia wanafunzi wake wenye miaka sita na saba kuwa hekaya nyengine kama ‘Tooth Fairy’ na ‘Easter Bunny’ pia ni za uongo. Easter Bunny ama Sungura wa Pasaka anaaminika kuwapatia watoto wema mayai na zawadi nyengine wakati wa pasaka, nayo huaminiwa sana na watoto.

Father Christmas na Easter Bunny ni hekaya ambazo zinalenga kuwafanya watoto kuwa watiifu na wenye adabu, na kuwaaminisha kuwa ukiwa mkaidi hautopata zawadi itakapowadia siku kuu. Ni sawa na usemi wa waswahili kuwa: ‘Makaidi hafaidi mpaka siku ya Idi’.

Tooth Fairy ni hekaya ambayo watoto wanaaminishwa baada ya kung’oa jino endapo wataliweka chini ya mto wa kulalia basi asubuhi hugeuka zawadi na pesa.

Lengo ni kuwafanya wasiogope na wawe na hamu ya kung’oa meno ili wapate zawadi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents