Burudani

Mwana FA akosoa mfumo wa Record label za Bongo

By  | 

Mwana FA amesema mfumo wa Record label hapa nchini bado haujawa katika kiwango kile kinachotakiwa kitu ambacho kinamfanya hata yeye kusita kuingia huko.

Mwana FA

Mwana FA amesema msanii akiwa anafanya muziki anatakiwa kutoka sehemu moja na kwenda kwingine, maana yake unakuwa msanii mdogo, wa kati, msanii mkubwa na baadae hata kuwa C.E.O.

“The way music industry yetu ilivyokuwa setup hakuna hata proper record label, ni kitu kama tutakuwa tunakifanya kienyeji mwishoni tutaishia kutukanana kama wasanii na mameneja wao mitaani,” Mwana FA ameimbia Clouds FM

“Ni kitu ambacho nakifikiria lakini kila wakati una hiki na hiki inakufanya unasita kidogo sababu huoni namna utafanya kazi katika mfumo ambao tunao; sio kitu ambacho na kiwrite off, kipo ila naangalia namna ambavyo mfumo wetu utaweza kukisapoti,” amesema Mwana FA.

By Peter Akaro

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments