Mwanafunzi awachoma kisu Walimu wawili kwa wakati mmoja (+ Video)

Edwin Mokaya, mwalimu katika Shule ya Kisii anasaidiwa na wauguzi Hospitali ya Ram baada ya kuchomwa kisu na mwanafunzi wa kidato cha tatu.
 Polisi inamshikilia mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu aliyewachoma visu walimu wawili katika shule ya upili ya Kisii. Mwanafunzi huyo alihojiwa na maafisa wa upelelezi kutoka ofisi za Kisii Central DCIO baada ya mmoja wa waathiriwa kurekodi taarifa.
Katika taarifa hiyo Polisi walisema wamepanga kumshtaki mwanafunzi huyo kwa shambulio hilo ambalo inaelezwa kuwa Mwanafunzi huyo alienda kutafuta kisu katika bweni hivyo alifanya makusudi, akakiweka kwenye soksi zake kabla ya kumchoma mmoja wa walimu ambao walikuwa wakimkemea kwa kuchelewa.
Mwanafunzi huyo alituhumiwa kwa kukataa kupiga magoti kabla ya kumshambulia Mwalimu huyo huku muathiriwa  wa pili alidungwa kisu wakati alijaribu kumwokoa mwenzake.
Walimu walioathiriwa walitambuliwa kama Edwin Mokaya na Elvis Maoto. Majeraha matatu ya kuchomwa Wawili hao walitibiwa katika Hospitali ya Ram katika mji wa Kisii. Msimamizi wa hospitali hiyo, Enock Abobo, alisema mmoja wa walimu atafanyiwa upasuaji.
Bofya hapa chini kulitazama tukio zima:

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW