Tupo Nawe

Mwanamitindo adondoka jukwaani na kufariki akiwa kwenye onyesho (Video)

Mwanamitindo wa kiume, Tales Soares (26) amefariki dunia baada ya kuanguka jukwaani wakati akitembea kwa mwendo wa maringo (catwalk) alipokuwa akishiriki kwenye wiki ya mitindo mjini São Paulo, nchini Brazil. Soares alipoanguka, watazamaji walidhani ni sehemu ya onesho lake.

Mwanamitindo huyo alipatiwa huduma ya kwanza na kufaliki muda mfupi baadae wakati akipelekwa hospitali. Kampuni ambayo ilikuwa inasimamia onesho hilo ilitumia mtandao wa twitter kutoa salamu za pole kwa ndugu na jamaa wa Tales.

Watazamaji waliokuwepo kwenye maonyesho hayo walidhani kuwa ni moja ya sehemu ya maonyesho baada ya kumuona Tales Soares ameanguka chini huku baadhi ya wanamitindo walionekana kuingiwa na hofu ndipo zimamoto walipojitokeza na kumkimbiza hospitalini.

Baada ya muda mchache waandaaji wa maonyesho hayo walitoa taarifa za kifo cha mwanamitindo huyo kupitia ukurasa wa twitter bila kutoa ufafanuzi juu ya kifo chake.

“Tunapenda kutoa pole kwa familia ya Tales kwa kumpoteza kijana wao, tutatoa mchango muhimu katika kipindi hiki kigumu” waliandika.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW